Skip to main content

Madhila ya watoto wasio na makazi nchini Burundi

Madhila ya watoto wasio na makazi nchini Burundi

Wakati bara la Afrika linaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika hii leo juni 16 , nchini Burundi kama mataifa mengi ya bara Afrika inakumbwa na changamoto ya idadi kubwa ya watoto wa mitaani wanaorandaranda mijini.

Taifa hilo linalopitia vipindi vya machafuko na vita limekuwa likishuhudia ongezeko la watoto wa mitaani kila uchao.

Sababu za ongezeko hilo ni nyingi lakini miongoni mwao ni Maisha duni ndani ya familia.

Mji mkuu Bujumbura pekee unakisiwa kuwa na watoto wa mitaani zaidi ya 2000 kati ya jumla ya 3500 wanaokadiriwa kuwa wa mitaani nchini Burundi. Serikali ya nchi hiyo imeanda sera ya kuwaondoa watoto hao mitaani lakini inakabiliwa na changamoto ya fedha. Kutaka Kujua upana wa tatizo hilo, ungana na mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani KIBUGA katika makala hii.