Skip to main content

MINUSMA pekee haiwezi kuleta amani Mali- UM

MINUSMA pekee haiwezi kuleta amani Mali- UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu hali ya amani na usalama nchini Mali, likipokea ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Ripoti imewasilishwa na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali,MINUSMA Mahamat Saleh Annadif ambapo amesema hali ya usalama imezidi kuzorota nchini Mali katika wiki za karibuni.

Raia na walinda amani wameuawa wengine wamejeruhiwa huku mali na miundombinu ya MINUSMA na hata vikosi vya ulinzi vya serikali ikiharibiwa hivyo amesema..

(Sauti ya Mahamat)

Baada ya kusema hayo, MINUSMA pekee haiwezi kutatua changamoto zote za usalama nchini Mali. Tena haikuundwa kukidhi hilo na hakuna ujumbe wowote wa ulinzi wa amani unaoweza kukidhi hilo. Suluhu ni kuongeza nguvu za vikosi vya ulinzi vya kitaifa vya Mali ili kutekeleza majukumu hayo ya kitaifa. Ndio maana tunaomba vikosi vya Mali visaidiwe. Kurejeshwa kwa mamlaka ya serikali kunategemea hilo.”