Skip to main content

ISIL yatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya wayazidi

ISIL yatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya wayazidi

Kundi la kigaidi la ISIL limethibitishwa kuwa limetekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa jamii ya Yazidi nchini Iraq, na bado mauaji yanaendelea. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Tume ya Uchunguzi ya Syria, ambayo mkuu wake Paulo Pinheiro amesema wanaume na wavulana wanauawa, wakati wasichana na wanawake wanauzwa kama watumwa wa kingono.

(Sauti ya Bwana Pinheiro)

“Mauaji ya kimbari yanaendelea. Kuanzia siku ya mashambulizi dhidi ya Sinjar hadi leo, ISIS imeendelea kujaribu kuwamaliza wayazidi kupitia mauaji, utumwa wa kingono, utumikishwaji, mateso na vitendo vilivyo dhidi ya ubinadamu pamoja na uhamisho uliosababisha maumivu ya kimwili na kisaikolojia.”

Kwa mujibu wa tume hiyo, ushaidi uliokusanywa unatosha kufungua mashtaka ya mauaji ya kimbari dhidi ya ISIL.

Jamii ya wayazidi ni kabila la watu takriban 400,000 wanaoishi kwenye eneo la Sinjar, kaskazini mwa Iraq, na ambao wameanza kushambuliwa na ISIL mwezi Agosti mwaka 2014.