Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango bila utashi wa kisiasa haitazaa matunda- Baraza

Mipango bila utashi wa kisiasa haitazaa matunda- Baraza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesihi nchi wanachama wa umoja huo kuongeza kiwango cha fedha kwenye miradi inayohusika na masuala ya wanawake, amani na usalama.

Taarifa ya Rais wa Baraza hilo iliyotolewa baada ya kikao kuhusu masuala ya wanawake, amani na usalama ikiangazia usafirishaji haramu wa binadamu kwenye mizozo, wajumbe wamesisitiza zaidi usaidizi hususan kwenye mizozo na baada ya mizozo.

Wajumbe wametambua kuanzishwa kwa chombo cha kuchagiza ushiriki wa wanawake kwenye amani, usalama na usaidizi wa kibinadamu, GAI kama njia mojawapo ya kupitisha fedha za kusaidia miradi ya kushirikisha kundi hilo.

Wametambua pia harakati za kikanda ikiwemo Muungano wa Afrika, AU za kuunda mpango wa jinsia, amani na usalama mwaka 2015-2020 sambamba na nchi kuandaa mipanog ya kitaifa ya kutekeleza uamuzi huo.

Hata hivyo wametaka utashi wa kisiasa, rasilimali, uwajibikaji na wataalamu wa sekta ya jinsia ili kufanikisha utekelezaji wa mipango hiyo.