Kongamano kuhusu albino barani Afrika ni mwanzo wa vuguvugu la mabadiliko: Dkt. Possi

Kongamano kuhusu albino barani Afrika ni mwanzo wa vuguvugu la mabadiliko: Dkt. Possi

Kuelekea kongamano la kwanza la kuchukua hatua kuhusu hatma ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino barani Afrika, ambalo litafanyika jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kuanzia Juni 17 hadi 19 Naibu waziri katika ofisi ya Waziri Mkuu nchini humo anayeshughulika na watu wenye ulemavu Dkt Abdalla Possi amesema mkutano huo ni fursa kubwa katika kusaka haki za kundi hilo.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii jijini New York, Marekani anakohudhuria mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu, Dkt Possi amesema hatua hiyo ya aina yake ni ishara kwamba harakati zimechukua sura mpya.

(SAUTI DKT. POSSI)

Amesema mauaji dhidi ya albino yamepungua ikilinganishwa na miaka ya hivi karibuni lakini bado safari ni ndefu kwani imani potofu hazijatokomea.

(SAUTI YA DKT. POSSI)