Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna matumaini kwa wakimbizi wa Somalia nchini Kenya

Kuna matumaini kwa wakimbizi wa Somalia nchini Kenya

Hatma ya wakimbizi wa Somalia walioko kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya inaonyesha matumaini. Hii ni baada ya ziara ya kamishina mkuu wa wakimbizi Filipo Grandi kuzuru Somalia na Kenya kujadili na viongozi wa nchi hiyo kuhusu suala hilo.

Grandi pia alipata fursa ya kukutana na wakimbizi waliorejea Somalia baada ya serikali ya Kenya kusema ina mpango wa kuifunga kambi hiyo, lakini pia wale walioamua kusalia kambini Dadaab. Kwa undani zaidi ungana na Flora Nducha katika makala hii.