Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda kutumia ndege zisizo na rubani kuwajengea uwezo wakimbizi: UNISDR

Uganda kutumia ndege zisizo na rubani kuwajengea uwezo wakimbizi: UNISDR

Uganda inaandaa ramani kwa makazi ya wakimbizi ambayo yanahifadhi maelfu ya watu katika taifa hilo la Afrika mashariki, lengo likiwa ni kusaidia habari za hatari kwa maendeleo na mipango ya matumizi ya ardhi hivyo kujenga uwezo wa jamii.

Mfano kuweka ramani ya makazi ya wakimbizi ya Oruchinga wilaya ya magharibi mwa Uganda ya Isingiro kutatoa ushahidi kwa miundombinu na miapango ya maendeleo , na kujumuisha taarifa za hali ya hewa na majanga ya asili. Hili litafanikiwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani yaani Drones.

Mradi huo anzilishi unaendeshwa na kitengo cha Uganda cha maandaalizi ya kukabili majanga, udhibiti na wakimbizi, ambayo ni sehemu ya ofisi ya waziri mkuu kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na chuo kikuu cha Maryland cha Marekani.

Kwa mujibu wa Steven Goldfich mshauri wa udhibiti wa hatari ya majanga kwenye shirika la UNDP, ramani hiyo kwa makazi ya wakimbizi itasaidia kuonyesha mahali, aina na usambaaji wa majanga , kama vile uvunaji wa mchanga unaotumika kwa ujenzi ambao unaweza kusababisha hatari ya mafuriko, ili kusaidia kufanya maamuzi.

Uganda hivi sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 500,000 na waomba hifadhi katika makazi mbalimbali nchini humo, na kwa mujibu wa shirika la wakimbizi UNHCR ni idadi kubwa kabisa kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.