Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vinywaji vyenye moto kupindukia vyaweza sababisha saratani- Utafiti

Vinywaji vyenye moto kupindukia vyaweza sababisha saratani- Utafiti

Unywaji wa vimiminika vyenye moto kupindukia unaweza kusababisha saratani ya njia ya kusafirisha chakula kutoka kooni hadi tumboni au umio kwa binadamu, umesema ufatifi uliochapishwa kwenye jarida la kitabibu la Lancet.

Utafiti huo uliendeshwa na wanasayansi 23 chini ya taasisi ya kimataifa ya utafiti wa saratani IARC ya Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO.

Wanasayansi hao walitakiwa kuangalia uwezekano wa kahawa na kinywaji kingine aina ya Matee kutoka Amerika ya Kusini pamoja na vinywaji vya moto sana iwapo vinaweza kusababisha saratani ambapo Kahawa na Matee utafiti itabidi kufanyika zaidi.

Dkt. Christopher Wild ni Mkurugenzi wa IARC.

(Sauti ya Dkt. Christopher)