Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s na ajenda ya Afrika ya 2030 havitengamani:UNDP

Ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s na ajenda ya Afrika ya 2030 havitengamani:UNDP

Mataifa ya Afrika yanajitahidi kuzijumuisha ajenda ya kimataifa ya maendeleo endelevu yaani SDG’s na ajenda ya maendeleo ya Afrika ya mwaka 2030.Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Hii ni kwa sababu ajenda hizi mbili hazitengamani na zinapaswa kwenda sanjari kuhakikisha hakuna anyesalia nyuma katika suala la maendeleo.

Kwa kumujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, nia ni kuziingiza ajenda zote mbili katika mipango, maendeleo, na sera za kitaifa na kikanda. Na katika hatua ya kwanza ya kusaidia maafisa wa serikali, asasi za kirasia na wadau wa maendeleo katika kujumuisha ajenda hizi mbili ,UNDP na serikali ya Kazakhstan imeandaa warsha ya siku mbili mjini Johanesburg Afrika ya Kusini na Darkar Senegal kwa ajili ya mataifa ya Afrika, kuanzia leo.

Miongoni mwa wanaohudhuria ni Bi Amina Shaaban , naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango wa Tanzania

(SAUTI YA AMINA SHAABAN)