Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lateua tume ya haki za binadamu Sudan Kusini

Baraza la haki za binadamu lateua tume ya haki za binadamu Sudan Kusini

Rais wa baraza la haki za binadamu balozi Choi Kyonglim ametangaza leo uteuzi wa Yasmin Sooka wa Afrika Kusini, Kenneth R. Scott wa Marekani na Godfrey M. Musila wa Kenya, kuwa wajumbe watatu wa tume ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini, ikiongozwa na Bi. Sooka. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Baraza la haki za binadamu liliamua kuunda tume ya haki za binadamu ya Sudan Kusini kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa lengo la kufuatilia njaa kutoa ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini, lakini pia kutoa mapendekezo ya kuboresha hali hiyo.

Wajumbe hao watatoa muongozo kwa serikali ya Sudan kusini, kuhusu masuala ya haki, uwajibikaji na masuala ya upatanishi, wakihusisha mikakati ya kimataifa na kikanda katika kuchagiza uwajibikaji wa ukiukaji wa haki za binadamu na ukatili.