Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha hatua za Guatemala kupambana na ufisadi na ukwepaji sheria

UM wakaribisha hatua za Guatemala kupambana na ufisadi na ukwepaji sheria

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imekaribisha hatua muhimu za kijasiri zilizochukuliwa wiki chache zilizopita na serikali ya Guatemalan katika kupambana na ufisadi na ukwepaji wa sheria.

Jumamosi iliyopita mawaziri wa zamani watatu walitiwa nguvuni na kushikiliwa kwa madai ya kujihusisha na biashara haramu ya fedha kinyume cha sheria.

Mawaziri wengine wawili wa zamani pia wako mbioni kukamatwa kwa mashitaka kama hayo, katika kesi ya ngazi ya juu inayomuhusisha Rais wa zamani wa nchi hiyo Molina na makamu wa zamani wa Rais Baldetti.

Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu mnamo Juni pili uongozi wa Guatemala pia uliwakamata watu 25 na kutoa vibali vya kukamatwa kwa watu wengine 27 kwa uchangiaji kinyume cha sharia fedha kwenye kampeni za chama cha Patriotic wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2011.

Ofisi hiyo inasema inatumai juhudi hizo za serikali kupambana na ufisadi na ukwepaji wa sheria , ikiwa ni pamoja na kufanyia marekebisho mfumo wake wa sheria na haki vitakuwa ni mfano wa kuigwa na mataifa mengine.