Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wanaosafiri bila wazazi wakabiliwa na hatari kubwa:UNICEF

Watoto wanaosafiri bila wazazi wakabiliwa na hatari kubwa:UNICEF

Watoto tisa kati ya 10 wahamiaji na wakimbizi wanaowasili Ulaya mwaka huu kupitia Italia wako pekee yao bila wazazi au walezi. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Taarifa ya Joshua)

Hali hii imefanya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kutoa onyo kufuatia ongezeko la vitisho vya ukatili, unyanyasaji na vifo vinavyowakabili.

Katika ripoti yake, “Hatari katika kila hatua njiani”, iliyotolewa leo UNICEF inasema watoto 7,009 walio peke yao walivuka bahari kutoka Afrika Kaskazini na kuingia Italia miezi mitano ya mwanzo wa mwaka huu, ikiwa ni idadi mara mbili ya mwaka jana.

Mmoja wao barubaru kutoka Libya amesema “ukijaribu kukimbia unapigwa risasi, ukiacha kufanya kazi unapigwa na kinachowasibu ni kama ilivyokuwa biashara ya utumwa, kama anavyofafanua Sarah Crowe msemaji wa UNICEF

 

(SAUTI YA SARAH CROWE)

“Baadhi yao watoto hawa wamekumbwa na kiwewe kiasi kwamba hawajaweza kusimulia kwa kina ni wakati gani walinyanyaswa au hata walikuwa wapi.”