Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kama ulemavu wa ngozi ni utajiri, wao wangalitajirika- Jane

Kama ulemavu wa ngozi ni utajiri, wao wangalitajirika- Jane

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kuhamasisha Jamii kuhusu haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumeanza mkutano wa siku tatu kuhusu watu wenye ulemavu. Joseph Msami na taarifa kamili.

(Taarifa ya Msami)

Mkutano huo unahusisha nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu, ambapo maudhui ni kuangazia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030.

Mmoja wa washiriki ni Jane Kihungi kutoka Kenya akiwakilisha mtandao wa wanawake wenye ulemavu barani Afrika ambapo nimemuuliza dhana potofu ya mauaji ya Albino.

(Sauti ya Jane)