Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni 168 bado wanatumikishwa: ILO

Watoto milioni 168 bado wanatumikishwa: ILO

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupambana na utumikishwaji wa watoto, Shirika la Kazi duniani ILO limesema kwamba bado tatizo hilo limeenea duniani kote, watoto milioni 168 wakiwa wanatumikishwa.

Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo, mkurugenzi wa ILO Guy Rider amesema kinachohitajika sasa ni sera zinazolenga elimu bora, huduma za kijamii na ajira zenye hadhi kwa wazazi.

Bwana Rider amesema utumikishwaji wa watoto hutokea hasa kwenye maeneo ya vijijini na katika sekta za uchumi zisizokuwa halali na ambapo hakuna viwango vya ajira, huduma wala ulinzi wa serikali, na ukisasababishwa na ukosefu wa kipato kwa wazazi wanaolazimishwa kutumikisha watoto wao.

Hata hivyo, bwana Rider amemulika jitihada za kampuni zinazojaribu kuchugunza ugavi wao ili kudhibiti vitendo vya utumikishwaji wa watoto.