Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon alaani shambulio la Orlando

Ban Ki-moon alaani shambulio la Orlando

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi ya kutisha sana yaliyotokea leo alfajiri mjini Orlando, Florida, nchini Marekani, ambapo zaidi ya watu hamsini wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ametuma salamu zake kwa familia za wahanga. Aidha ameeleza mshikamano wake na serikali na raia wa Marekani.