Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ladsous atembelea Sudan Kusini kutathmini mchakato wa amani

Ladsous atembelea Sudan Kusini kutathmini mchakato wa amani

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa , Hervé Ladsous, amewasili nchini Sudan Kusini kutathimini hali kufuatia kuundwa kwa serikali ya mpito na umoja wa kitaifa pamoja na ahadi ya usaidizi ya UM kupitia ujumbe wake nchini humo UNMISS .

Akiongea muda mfupi baada ya kwasili mjini Juba, Ladsous amesema kile atakachokipa kipaumbele katika ziara yake hiyo.

(SAUTI LADSOUS)

‘‘Kuona pale tulipofikia kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya amani, muundo wa serikali ya mpito, na kuwasikiliza watu.’’