Msafara wa kwanza wa chakula wakamilisha kufikisha msaada Daraya:OCHA
Msafara wa kwanza wa kufikisha msaada wa chakula mjini Daraya Syria umekamilisha kazi kwa mafanikio umesema Umoja wa Mataifa Ijumaa.
Chakula cha kuwatosha watu 2000 kwa muda wa mwezi mmoja kiliwasili kwa malori 79 katika operesheni iliyofanyika usiku kucha limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. Msemaji wa shirika hilo ni Jens Laerke.
(SAUTI YA JENS LAERKE)
“Tumefurahi saana kwamba hatimaye tumeweza kufikisha msafara wa pamoja wa Umoja wa mataifa, na jumuiya ya Syria ya mwezi mwekundu mjini Daraya, mji ambao haukuweza kuona chakula tangu 2012.”
OCHA inasema ni muhimu kuendelea kupata fursa ya kuingia sio tu Daraya bali katika maeneo yote yanayozingirwa na yaliyo vigumu kufikika Syria, ambako watu milioni 4.6 wanahitaji msaada wa haraka baada ya miaka mitano ya vita.