Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid aonya Isarel kulipiza kisasi Palestina

Zeid aonya Isarel kulipiza kisasi Palestina

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa , Zeid Ra’ad Al Hussein ameonya kuwa hatua ya Israel kulipiza kisasi dhidi ya Palestina kufuatia shambulio la kigaidi yaweza kuathiri maelfu ya Wapalestina.

Akongea mjini Geneva Kamishina Zeid ambaye alilaani sahmbulio hilo amesema itakuwa ni adahbu jumuishi huku akikosoa uamuzi wa mamlaka ya Israel kusitisha vibali 80,000 vya kusafiria kwa wakazi wa ukiongo wa mto Magahraivina Gaza.

Amesema hatau hiyo huwaadhibu maelfu ya raia watu wasio na hatia.

Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR.

(SAUTI RAVINA)

"Hii ni idadi kubwa kabisa ya vifo vya Waisrael tangu mfululizo wa mashambulizi. Tunasikitishwa kadhalika na malipizo ya mamlaka Israel, ambayo yanahusisha hatua ambazo zitaadhibu wengi na kuongeza madhila wanayopitia Wapalestina wakati huu wa mvutano.’