Skip to main content

Hatua zimepigwa katika mapambano dhidi ya ukimwi,juhudi zaidi zahitajika:Dr Kigwangalla

Hatua zimepigwa katika mapambano dhidi ya ukimwi,juhudi zaidi zahitajika:Dr Kigwangalla

Serikali ya Tanzania imesema imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya ukimwi, lakini mafanikio hayo hayatakuwa na maana endapo watabweteka. Hayo yamesemwa na naibu waziri wa afya wan chi hiyo Dr Hamis Kigwangalla alipoketi na kuzungumza na Flora Nducha wa idhaa hii.

Pia amesema changamoto kubwa waliyonayo ni rasilimali fedha, sasa wameunda mkakati kabambe kuhakikisha wanazipata na kusukuma mbele mchakato wa kufikia lengo la kutokomeza ukimwi ifikapo mwaka 2030 kama sehemy ya utekelezaji wa maendeleo endelevu yaani SDG’s.

Ungana nao katika mahojiano haya ambapo Dr Kigwandala anaanza kunyambua mafanikio waliyofikia

(MAHOJIANO NA DR KIGWANGALLA)