Harakati za kudhibiti Ukimwi na VVU zaanza kuzaa matunda Afrika

9 Juni 2016

Uganda, Burundi na Tanzania ni miongoni mwa mataifa 21 barani Afrika ambayo yametajwa kuwa na mafanikio ya aina yake ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa watoto halikadhalika kwa wajawazito.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaofanyika New York, Marekani na mada kuu ikiwa Ukimwi, #HLM2016AIDS ambapo nchi hizo zinatajwa kuwa ni miongoni mwa zilizokuwa zimetikiswa zaidi na Ukimwi.

Taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti ukimwi, UNAIDS na mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kukabili Ukiwmi, PEPFAR, imesema maambukizi mathalani kwa watoto yamepungua kwa asilimia 60 tangu mwaka 2009 ulipoanzishwa mpango wa kimataifa.

Halikadhalika katika nchi hizo, asilimia 80 ya wajawazito wanaoishi na virusi vya Ukimwi wanapatiwa dawa ili kudhibiti maambukizi hayo kwa watoto wao, halikadhalika kupunguza makali ya virusi.

Wakati a uzinduzi wa ripoti hiyo, UNAIDS, PEPFAR na wadau wamezindua pia mfumo mpya wa kuharakaisha mipango ya kutokomeza Ukimwi miongoni mwa watoto, barubaru na vijana wa kike.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter