Mtaalam wa haki za binadamu kuzuru tena CAR

9 Juni 2016

Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Marie-Thérèse Keita Bocoum, atafanya ziara nyingine nchini humo kuanzia Juni 10 hadi 20 mwaka huu wa 2016.

Ziara yake hiyo ya saba nchini CAR inafuatia kuapishwa kwa serikali mpya iliyoundwa na Rais Touadéra, na kuanza kazi kwa wabunge wapya waliochaguliwa nchini humo.

Bi Keita Bocoum amesema anaenda kujadiliana na mamlaka za CAR, wawakilishi wa kiraia, na jamii ya kimataifa kuhusu hali ya haki za binadamu, masuala ya usalama, kuheshimu haki za binadamu, masuala ya sheria, na maridhiano ya kitaifa.

Mtaalam huyo huru anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake ya mwisho kwa Baraza la Haki za Binadamu mnamo Septemba 2016.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter