Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola Liberia

WHO yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola Liberia

Leo Shirika la Afya Duniani(WHO) limetangaza kumalizika rasmi kwa mlipuko wa karibuni wa virusi vya Ebola nchini Liberia. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Tangazo hili limekuja siku 42 baada ya ya kuthibitisha kisa cha mwisho cha mgonjwa wa Ebola kupimwa kwa mara ya pili na kukutwa hana virusi vya ugonjwa huo nchini humo.

Liberia sasa inaingia katika siku 90 za uangalizi ili kuhakikisha kwamba kisa chochote kipya kinabainika haraka na kudhibitiwa kabla mlipuko haujaanza kusambaa.

Liberia ilitangaza kwa mara ya kwanza kutokomeza Ebola 9 Mei 2015 lakini virusi hivyo vikaibuka tena.