Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika iwekeze katika kukabiliana na El Niño, mabadiliko ya tabianchi: Kamau

Afrika iwekeze katika kukabiliana na El Niño, mabadiliko ya tabianchi: Kamau

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya El Niño na mabadiliko ya tabianchi Baliozi Macharia Kamau  amesema kazi kubwa aliyo nayo ni kuhakikisha nchi za Afrika zinajenga uwezo wa kukabiliana na na madhara El Niño.

Mteule huyo wa hivi karibuni ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika ofisi yaUmoja wa Mataifa mjini New York, ameimabia idhaa hii katika mahojiano maalum kuhusu nafasi hiyo kuwa ni dhahiri Afrika imeathiriwa zaidi na El Niño lakini hata mataifa yaliyoendelea kama Ufaransa yamethiriwa kwahiyo.

( SAUTI KAMAU)

Amesema elimu zaidi inahitajika kwa raia juu ya namna ya kukabliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi na El Niño.