Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani vikali shambulio la kigaidi Tel Aviv

Ban alaani vikali shambulio la kigaidi Tel Aviv

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi la jana usiku mjini Tel Aviv Israel ambalo limekatili maisha ya Waisrael wanne na wengine wengi kujeruhiwa.

Shambulio hilo limetelekezwa na wauaji wa Kipalestina . Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali ya Israel.

Katibu mkuu amerejelea msimamo kwamba hakuna sababu yoyote ya kuhalaluisha ugaidi na wala kwa wale wote wanaotekeleza vitendo hivyo vya kihalifu.

Ban ameshangazwa saana kwamba viongozi wa Hamas wamechagua kukaribisha shambulio hilo na wengine kulisherehekea. Ameutaka uongozi wa Palestina kutekeleza wajibu wake wa kusimama kidete dhidi ya ghasia na vitendo vinavyochochea ghasia hizo.