Skip to main content

Tanzania licha ya kujivunia mafanikio, bado kuna changamoto katika vita dhidi ya ukimwi:Kigwangalla

Tanzania licha ya kujivunia mafanikio, bado kuna changamoto katika vita dhidi ya ukimwi:Kigwangalla

Mkutano wa ngazi ya juu wa baraza kuu la Umoja wa mataifa leo unaendelea kwa nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, kuelezea mikakati yao baada ya kupitishwa azimio la kuhakikisha ukimwi unatokomezzwa ifikapo mwaka 2030.Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Tanzania ni miongoni mwa mataifa 21 barani Afrika ambayo yametajwa kuwa na mafanikio ya aina yake ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa watoto halikadhalika kwa wajawazito.

Kwenye mkutano huu inawakilishwa na naibu waziri wa afya Dr Hamis Kigwangalla ambaye amesema wamepiga hatua kubwa katika nyanja nne ya vita dhidi ya ukimwi ikiwemo kuenea, kutoa tiba, kupunguza athari na unyanyapaa, lakini pia kusaidia watoto yatima walioachwa.

Akizungumza na idhaa hii kuhusu mikakati ya kufikia lengo la kutokomeza ukimwi mwaka 2030 kwa Tanzania amesema..

(KIGWANGALLA CUT 1)

Amesema changamoto kubwa kwao ni fedha lakini wana mkakati..

(KIGWANGALLA CUT 2)