Jamii nzima inahitaji kujihusisha na upunguzaji wa majanga:UNISDR

Jamii nzima inahitaji kujihusisha na upunguzaji wa majanga:UNISDR

Jamii nzima inahitaji kujihusisha na masuala ya upunguzaji majanga endapo tunahitaji kufanikiwa katika suala hilo amesema mkuu wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya upunguzaji wa hatari ya majang UNISDR.

Bwana Robert Glasser ameyasema hayo alipozungumza mjini Asuncion, Paraguay wakati mawaziri na wajumbe kutoka mataifa yote ya Amerika wakikutana kujadili jinsi gani ya kutekeleza makubaliano ya kimataifa ya kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na majanga ya asili kwenye ukanda huo.

Ukanda huo umekuwa ukikumbwa na idadi kubwa ya majanga ya asili ikiwemo matetemeko ya ardhi, milipuko ya volcano, ukame , vimbunga na mafuriko yaliyosababishwa na El Nino.

Bwana Glasser amesema ili kuweza kukabili hayo mtazamo wenye wigo mpana zaidi ujulikanao kama DDR unahitajika ili kupunguza hatari ya majanga.