Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maambukizi ya VVU kwenda kwa mtoto yaanza kudhibitiwa Tanzania

Maambukizi ya VVU kwenda kwa mtoto yaanza kudhibitiwa Tanzania

Kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua nchini Tanzania kutokana na jitihada za serikali zilizojumuisha jumuiya ya kimataifa. Jitihada hizo ni pamoja na wanandoa kupatiwa mbinu za kuepusha maambukizi hata kutoka kwa mmoja wao mwenye virusi. Na kuthibitisha hilo tunaelekea mkoani Kagera nchini humo ambako Nicholas Ngaiza anakuletea makala kuhusu kisa cha wanandoa ambao mmoja alipata maambukizi ya VVU na wakaendelea na uhusiano bila kumuambukiza mwenzake huku pia mtoto akizaliwa salama. Kulikoni? Ungana naye.