Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tudhamirie kutunza na kutumia bahari kwa njia endelevu- Ban

Tudhamirie kutunza na kutumia bahari kwa njia endelevu- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ametoa wito wa kudhamiria upya kutunza na kutumia bahari na rasilmali zake kwa njia ya amani na endelevu kwa vizazi vijavyo.

Ban amesema hayo katika taarifa ya ujumbe wake leo Juni 8, ikiwa ni siku ya bahari duniani.

Aidha, ameongeza kuwa ili kutunza ubora wa bahari, ni vyema kufahamu hali yake sasa, na kuelewa athari za vitendo vya mwanadamu na mabadiliko ya tabianchi dhidi yake.

Katibu Mkuu amesema bahari zilizotunzwa vyema ni muhimu kwa kuendeleza maisha kwenye sayari dunia, akitaja baadhi ya faida za bahari iliyotunzwa vyema, mathalan kudhibiti tabianchi, kuzalisha chakula chenye lishe bora, na kuwa chanzo cha ajira zinazonufaisha mamilioni ya watu.