Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aunga mkono HRW kuhusu haki za binadamu CAR

Ban aunga mkono HRW kuhusu haki za binadamu CAR

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ameeleza kusikitishwa na hali ya ukwepaji sheria katika ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa kamili na Flora Nducha

(Taarifa ya Flora)

Ban amesema hayo katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, kufuatia kutolewa ripoti ya shirika linalotetea haki za binadamu, Human Rights Watch, kuhusu hali nchini CAR.

Kuhusu madai dhidi ya walinda amani wa Jamhuri ya Kongo Brazzaville, Ban amesema anatarajia kuwa serikali ya Jamhuri ya Kongo itahakikisha kuwa waliohusika na vitendo hivyo vya uhalifu wanawajibishwa kisheria.