Skip to main content

DRC: MONUSCO yaathiriwa pia na hali ya usalama

DRC: MONUSCO yaathiriwa pia na hali ya usalama

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) umeathiriwa pia na ukosefu wa usalama mashariki mwa DRC, amesema leo msemaji wake Charles Bambara akizungumza na waandishi wa habari. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Hii na kwa mujibu wa akaunti ya Twitter ya MONUSCO, ikiwa inajibu swali la mwanahabari kuhusu uwezo wa MONUSCO wa kurejesha hali ya usalama mashariki mwa nchi.

MONUSCO imesema kwamba operesheni ya usalama ambayo inatekelezwa kwa ushirikiano na jeshi la kitaifa FARDC imeshaanza kuleta mafanikio na ni dalili nzuri ya ushirikiano mzuri baina ya MONUSCO na serikali.

Aidha MONUSCO imekariri kwamba waasi wanapigana vita vya aina tofauti, wakiwa wanajificha na kutumia udhalilishaji, na suluhu ikiwa ni ushiriki zaidi wa raia.

Hatimaye MONUSCO imesema iko tayari kusindikiza waasi wa FDLR mpaka Rwanda, lengo lake likiwa ni kusaidia serikali kutatua mzozo.