Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada za pamoja zahitajika kutokomeza ukimwi ifikapo 2030:Sidibe

Jitihada za pamoja zahitajika kutokomeza ukimwi ifikapo 2030:Sidibe

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limeanza Jumatano kikao cha ngazi ya juu kujadili suala la ukimwi. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Mjadala unajikita katika umuhimu wa kuongeza juhudi za vita dhidi ya ukimwi kwa miaka mitano ijayo ili kuiweka dunia katika msitari wa kutokomeza kabisa maradhi hayo ifikapo mwaka 2030 katika sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.

Rais wa Baraza Kuu Mogens Lykketoft akifungua amesema ni ajabu Ukimwi kuendelea kuwa tatizo katika dunia ya sasa yenye fursa za kuweza kutokomeza.

Akizungumzia suala hilo na wito kwa nchi wanachama Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na vita dhidi ya Ukimwi UNAIDS, Michel Sidibe amesema juhudi za pamoja zinahitajika na kwamba

(SAUTI YA SIDIBE)

"Tafadhali tunahitaji kuitumia miaka mitano ijayo ni fursa, na kama tutaikosa fursa miaka hiyo mitano, tutakuwa na zahma katika ugonjwa huu, tutakuwa na changamoto, na kama hatutolipa gharama sasa basi tultalipamaisha yetu yote”

Mwisho wa mjadala huo nchi wanachama wanatarajiwa kupitisha azimio la kisiasa kutokomeza ukimwi,ili kuongeza mchakato wa hatua zilizopigwa na kufikia malengo kwa wakati maalumu.