Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na ILO washirikiana kukomesha ajira ya watoto katika kilimo

FAO na ILO washirikiana kukomesha ajira ya watoto katika kilimo

Kuelekea siku ya kimataifa ya kupinga ajira ya watoto Juni 12,shirika la chakula na kilimo FAO na shirika la kazi duniani ILO wamezindua kozi maalum ya kuelimisha kuhusu umuhimu wa kupinga utumikishwaji wa watoto katika kilimo.

Kozi hiyo ni mahsusi kwa watunga sera za masuala ya kilimo na wadau wengine, ili kuhakikisha hatua za kupinga utumikishwaji kwa watoto zinajumuishwa katika mipango ya kilimo na maendeleo vijijini.

Bernd Seiffert ni afisa wa FAo anayehusika na taasisi za maendeleo vijijini anaelezea kosi hiyo itasaidiaje?

(SAUTI YA BERND SEIFFERT)

''Wadau wa kilimo, wanaweza kuungana na wadau wengine kama vile wa ajira, elimu, na wale wa ulinzi wa watoto kuwajibika katika jukumu hili muhimu la kuzuia utumikishwaji wa watoto.''