Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mwanahabari Salad Osman, Somalia

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mwanahabari Salad Osman, Somalia

Mkurungenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Irina Bokova, amelaani vikali kuuawa kwa mwanahabari Sagal Salad Osman nchini Somalia, mnamo Juni 5, 2016.

Katika taarifa, Bi Bokova amesema ukatili kamwe haukubaliki, na kwamba inatia uchungu hata zaidi unapotumiwa kumnyamazisha mwanamke ambaye ameonyesha ujasiri mkubwa kwa kufanya kazi muhimu katika mazingira magumu.

Sagal Osman, ambaye alikuwa mtangazaji katika kituo cha televisheni na radio ya kitaifa, aliuawa kwa kupigwa risasi mnamo Juni 5 magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu