Skip to main content

Wanafunzi waachiliwa kwa muda Burundi:UNICEF

Wanafunzi waachiliwa kwa muda Burundi:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) limepongeza uamuzi wa kuruhusu kuachiliwa kwa muda watoto sita waliokuwa wanashikiliwa katika magereza ya Muramvya nchini Burundi.

UNICEF imeomba watoto wote 11 ambao ni wanafunzi waachiliwe ili kufaulu mitihani yao ya mwisho wa mwaka kwa usalama.

UNICEF imesema nafasio ya mtoto ni kuwa shule na nyumbani na familia yake lakini asilani sio kwenye jela ya watu wazima. Imesema ni lazima watoto wote waruhusiwe kusoma na kufaulu mitihani yao katika mazingira salama na yanayostahili.