Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ili kutokomeza ukimwi 2030 , tuchukue hatua haraka sasa:Fedotov

Ili kutokomeza ukimwi 2030 , tuchukue hatua haraka sasa:Fedotov

Mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu kutokomeza ukimwi umeanza leo Jumatano hapa New York ukiwaleta pamoja viongozi wa dunia, asasi za kiraia na wadau wengine muhimu.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kupitisha azimio la kisiasa kuhusu kutokomeza ukimwi kama njia ya kuongeza mchakato na kufikia malengo ya kupambana na ukimwi kimataifa.

Hatua hizi zitaonyesha msisitizo wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi ifikapo mwaka 2030 kama sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC kama mdhamini mwenza shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS inazisaidia nchi katika kuimarisha fursa ya kuzuia, kutibu na kuhudumia watu wanaotumia mihadarati, na walioko magerezani.Watu ambao mara nyingu husahaulika katika vita dhidi ya ukimwi.

Akizungumzia suala hili mkuu wa UNODC Yury Fedotov amesema endapo tunataka kutokomeza ukimwi ifikapo 2030 ni lazima kuhuchua hatua za makusudi haraka na sasa kwa kutoa kipaumbele na kuwekeza katika njia zinazofaa kwa watu wanaotumia mihadarati na walio jela.