Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulizi huko Uturuki

Ban alaani shambulizi huko Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la leo la kigaidi lililofanyika huko Istanbul Uturuki na kusababisha vifo vya watu wapatao 11 na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Msemaji wa Ban amemnukuuu akisema ni matumaini yake wahusika wa shambulio hilo linalodaiwa kutokana na bomu lililotegwa kwenye gari, watabainika na kufikishwa mbele ya sheria.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa huku akiwatakia majeruhi ahueni ya haraka.

Amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa uko na mshikamano na wananchi wa Uturuki na serikali yao wakati huu wa kipindi hiki kigumu cha majonzi.