Skip to main content

FAO, China kuimarisha ushirikiano na nchi za kusini

FAO, China kuimarisha ushirikiano na nchi za kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, na serikali ya China wametangaza leo kuimarisha ubia wao na ushirikiano kati ya nchi za kusini.

Taarifa ya FAO inasema kuwa baada ya miongo ya mafanikio China na FAO wamekubaliana kupanua wigo wa ushirikiano wao kwa lengo la kukuza maendeleo vijijini kote duniani.

Makubaliano baina pande mbili kuhusu kilimo na uhakika wa chakula yamefikiwa Jumamosi ambapo taarifa ya FAO imefafanua kuwa yatasaidia katika kuosngesha mkakati wa China kusaidia brani Afrika na Amerika.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema ushirikiano huo unafungua mlango wa ubia zaidi katika kutatua changamoto za maendeleo ya kilimo, magonjwa yanayovuka mipaka, uvumbuzi wa kisayansi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na teknolojia ya habari na mawasiliano.