Skip to main content

Mashirika ya kimataifa yatoa wito kuhusu uchaguzi DRC

Mashirika ya kimataifa yatoa wito kuhusu uchaguzi DRC

Umoja wa Mataifa umewasihi wadau wa kisiasa kushirikiana ili kufanikisha mazungumzo ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

Taarifa iliyotolewa kwa pamoja na Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika AU, Muungano wa Ulaya EU na muungano wa nchi zinazozungumza kifaransa, OIF imemulika umuhimu wa kufikia maelewano ili kuandaa uchaguzi wa baadaye mwaka huu ulio huru, wa wazi na utakaoaminika.

Mashirika hayo yamesisitiza kuwa lengo ni kutunza amani na utulivu nchini humo, pamoja na utawala wa sheria na mchakato wa demokrasia.

Taarifa imetangaza pia kuundwa kwa kundi maalum la kuhamasisha mazungumzo hayo likiunganisha wawakilishi wa pande AU, EU, OIF , na mashirika ya kikanda ikiwemo SADC.

Aidha wameomba wafungwa wa kisiasa waachiliwe huru, na haki zote za kibinadamu ziendelee kulindwa na serikali.