Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nane kati ya watoto 10 hatarini kudhalilishwa kingono mitandaoni- UNICEF

Nane kati ya watoto 10 hatarini kudhalilishwa kingono mitandaoni- UNICEF

Vijana wanane kati ya 10 wenye umri wa miaka 18 wanaamini kuwa vijana wako katika hatari ya ukatili wa kingono au kuonewa kwenye mtandao, na zaidi ya watano kati ya 10 wanafikiri rafiki zao wanashiriki katika tabia za hatari wanapotumia intaneti. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Nats up and hold under…

Hii ni video iliyochapishwa sanjari na utafiti utafiti mpya uliofanywa na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Utafiti huo “Hatari na uwezekano:kukulia mtaandaoni” unatokana na kura ya maoni ya kimataifa iliyohusisha vijana zaidi ya 10,000 wenye umri wa miaka 18 kutoka mataifa 25, na yakibaini mtazamo wao kuhusu hatari inayowakabili wanapokuwa katika dunia hii iliyo sasa kama kijiji.

Katika video hii Alyn, si jina lake halisi, mtoto mwenye umri wa miaka 12 kutoka Ufilipino ni shuhuda wa ukatili wa kingono kupitia intaneti na sasa amenasuliwa.

Nats.. out

Clara Sommarin, ni mtaalamu wa masuala ya ulinzi wa mtoto, UNICEF.

(Sauti Clara)

Wakati awali tukiwaza kwamba watoto walio katika hatari zaidi ya ukatili mtandaoni ni wale kutoka nchi zilizoendelea kwa sababu labda wana kipakatarishi au simu, sasa tunafahamu kwamba hivyo sivyo, kwa uhakika watoto walio katika mazingira ya kipato cha  chini wako katika hatari sawa.”