Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rununu zasongesha maendeleo Afrika : Balozi Kamau

Rununu zasongesha maendeleo Afrika : Balozi Kamau

Mkutano wa kwanza wa wadau unaongazia nafasi ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi ukiingia siku ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, imeelezwa kuwa simu za viganjani au rununu ni miongoni mwa teknolojia inayosongesha maendeleo endelevu SDGS barani Afrika,

Hiyo ni kwa mujibu wa mwenyekiti mwenza wa Balozi Macharia Kamau ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York.

Akihojiwa na Idhaa hii amesema sayansi, teknolojia na uvumbuzi ni fursa kubwa ya kukuza maendeleo katika sekta kadhaa kama vile elimu, afya na an fedha.

( SAUTI KAMAU)

Akizungumzia mchango wa sayansi na teknolojia katika uhakika wa chakula amesema.

( SAUTI KAMAU)