Wanaokimbia Fallujah wahudumiwe kwa mujibu wa sheria: Zeid
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amezitaka mamlaka nchini Iraq kuchukua hatua kuhakikisha watu wanaokimbia mji wa Fallujah uliozingirwa na wapiganaji wa kikundi kinachotaka kuweka dola ya kiislamu ISIL wenye msimamo mkali, wanahudumiwa kulingana na sheria za kimataifa.
Kamishna Zeid amesema watu hao wanakumbaan na madhila kadhaa wakati wakikimbia eneo hilo na hukumbana na hali mbaya zaidi wakifika eneo jingine.