MINUSCA yajutia kifo cha raia aliyepigwa risasi na kikosi cha ulinzi wa Rais
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, MINUSCA, umeelezea masikitiko yake kufuatia kifo cha raia mmoja kilichotokea Juni tano katika tukio ambapo kikundi cha wafuasi walikikimbilia kikosi cha MINUSCA kinachofanya kazi za usalama wa Rais.
Katika mabishano raia mmoja aliuwawa baada ya kupigwa na risasi . MINUSCA imesema kwamba uchunguzi ulifanyika haraka kubaini mazingira ya kifo hicho.
Ujumbe huo umesema kufuataia maoni ya vyanzo mbalimbali, unafafanua kuwa kifo cha raia huyo hakina uhusiano wowote na masuala ya kidini na kwamba utatoa taarifa kuhusu tukio hilo haraka iwezekanavyo.