50,000 wakimbia Niger baada ya kushambuliwa na Boko Haram
Melfu ya watu wamekimbia nyumba zao kusini kaskazini mwa Niger kufuatia mfululizo wa mashambulizi toka kwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram walioko mjini Bosso mkoa wa Diffa.
Mashambulizi hayo yalianza Ijumaa, Jumapili na Jumatatu na hadi hii leo hali mjini Bosso bado ni tete. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lilionya mapema mwezi uliopita kwamba hali ya usalama katika mkoa huo ni mbaya na shirika hilo halijaweza kuhudumia moja kwa moja eneo hilo tangu Feberuari mwaka jana, wapiganaji wa Boko Haram walipoingia kutoka Nigeria.
Shirika hilo limesema limekuwa likitoa msaada katika eneo hilo kupitia wadau wa mashinani na kwamba timu ya dharura inatarajiwa kuweka kambi mkoani Diffa juma hili.
Adrian Edwrads ni msemaji wa UNHCR..
(SAUTI ADRIAN)
‘‘Machafuko yameenea kote mkoani Bosso mwezi Mei ikiwamo mauaji ya Mei 31 karibu na mji wa Yebi yaliyoacha watu tisa wakiwa wamefariki na kulazimisha wakazi karibu 50,000 na wakimbizi wa ndani kusaka malazi Bosso.’’