Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi zafanyika kupunguza idadi ya watu wanaoathirika na majanga

Juhudi zafanyika kupunguza idadi ya watu wanaoathirika na majanga

Juhudi zinafanywa na Umoja wa mataifa ili kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watu wanaoathirika na majanga ya asili na yanayosababishwa na binadamu, kutoka milioni 100 walioathirika mwaka jana.

Watu hao ni pamoja na zaidi ya milioni 50 ambao walikabiliwa na ukame. Mafuriko, tetemeko la ardhi na vimbunga vimesababisha madhara makubwa kwa mamilioni ya watu.

Wataalamu wanakutana wiki hii nchini Paraguay kujadili jinsi gani hatari hiyo inaweza kupunguzwa katika mataifa ya Amerika. Dr Robert Glasser ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari ya majanga (UNISDR).

(SAUTI YA ROBERT GLASSER)

“Kukabili hatari ya majanga ni moja ya njia inayoonekana kuleta mabadiliko katika maisha ya mamilioni ya watu wasiojiweza duniani ambao hali yao inazidi kuwa mbaya kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, ongezeko la idadi ya watu na kwa sababu nchi hazijumuishi hatari ya majanga katika chaguo la uwekezaji zinaoufanya.”