Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Mwakilishi wa EU; wajadili uhamiaji, Mashariki ya Kati, na hali Afrika

Ban akutana na Mwakilishi wa EU; wajadili uhamiaji, Mashariki ya Kati, na hali Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Bi Federica Mogherini, ambaye ni Mwakilishi Mwandamizi wa Muungano wa Ulaya (EU) kuhusu masuala ya kidiplomasia na usalama, na pia Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Ulaya.

Katika mkutano huo, wamejadili kuhusu masuala mbalimbali yanayogusa Umoja wa Mataifa na EU, mathalan Suala la Israel na Palestina, Syria, Libya, yemen, Afghanistan, uhamiaji, na kuhusu hali katika maeneo kadhaa ya bara Afrika.

Katibu Mkuu ameishukuru EU kwa ushirikiano wake, na kwa kuunga mkono kwa dhati Umoja wa Mataifa na juhudi zake katika masuala waliyojadili.

Kwingineko kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Bi Mogherini amehutubia Baraza la Usalama katika kikao chake kinachomulika ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na jumuiya za kikanda, ukiangazia EU.