Sayansi, teknolojia na ugunduzi ni muhimu kwa ajenda 2030- Ban
Mkutano wa kwanza wa wadau mbali mbali unaoangazia matumizi ya sayansi, teknolojia na ugunduzi ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs umefanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Assumpta Massoi na taarifa kamili.
(Taarifa ya Assumpta)
Akihutubia washiriki, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema sayansi, teknolojia na ugunduzi ni zaidi ya teknolojia mpya au programu za kompyuta, kwa kuwa ubunifu ni fikra na mtazamo.
Amesema mambo hayo matatu yanahuisha kuhoji fikra, kufikiria mifumo mipya na kanuni za utendaji pamoja na kuanzisha mikakati mipya, akisema kuwa teknolojia mpya ni muhimu kama njia ya kufanikisha mambo hayo, hivyo amesema..
“Kujumuisha sayansi, teknolojia na ugunduzi katika maendeleo endelevu mashinani ndiyo changamoto kubwa. Sayansi, teknolojia na ugunduzi ni lazima viwe njia ya kujumuisha jamii nzima, kuondoa umaskini na kuleta maendeleo endelevu.”