Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya kimataifa yazindua kipimo kwa uharibifu wa chakula

Mashirika ya kimataifa yazindua kipimo kwa uharibifu wa chakula

Kipimo sanifu cha kimataifa cha kupima utupaji na uharibifu wa chakula kimezinduliwa katika kongamano la ukuaji unaojali mazingira jijini Copenhagen, Denmark. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Kipimo hicho sanifu ni matokeo ya ubia wa mashirika ya kimataifa, yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa, mathalan lile la Chakula na Kilimo (FAO) na Shirika la Mpango wa Mazingira (UNEP).

Kipmo hicho ndicho cha kwanza kabisa cha aina yake, na kitatoa vigezo kwa kampuni na serikali ili ziweze kupima kwa njia inayoaminika na kuripoti uharibifu na utupaji wa chakula.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, Achim Steiner, ametoa wito kwa nchi na kampuni zitumie kipimo hicho, sambamba na hatua za kutimiza lengo dogo la SDG linalohusu kupunguza kwa nusu utupaji wa chakula ifikapo mwaka 2030.