Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutalinda amani DRC, wananchi mtuamini: IGP Bisengimana

Tutalinda amani DRC, wananchi mtuamini: IGP Bisengimana

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, polisi nchini humo imesema imejiandaa vyema kuhakikisha amani na usalama kabla, wakati na baada ya zoezi hilo.

Katika mahojiano na idhaa hii wakati akihudhuria mkutano wa ulinzi wa amani uliowaleta pamoja wa wakuu wa polisi kote duniani, Mkuu wa polisi DRC IGP Charles Bisengimana amesema kikosi chake kiko tayari kwa uchaguzi.

(SAUTI BISENGIMANA)

Kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO hivi karibuni kimefanya mafunzo kwa polisi wa DRC ili kuhakikisha amani wakati wa uchaguzi mkuu uinaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.