Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama bado ni tete Darfur:UNAMID

Hali ya usalama bado ni tete Darfur:UNAMID

Hali ya usalama kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan bado ni tete kufuatia mapigano yanayoendebaina ya majeshi ya serikali ya SAF na makundi ya waasi.

Hayo ni kwa mujibu wa naibu mwakilishi wa pamoja wa mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika kulinda amani Darfur UNAMID, anayehusika na masuala ya kisiasa Kingsley Mamabolo.

Akizungumza baada ya ziara ya siku tatu Mashariki mwa Darfur, amesema uhalifu unaendelea, wahanga wakiwa raia huku mashambulizi dhidi ya UNASMID nayo yakitokea mara kwa mara.

Ameongeza kuwa wafanyakazi wa UNAMID mara kadhaa wananyimwa fursa kuwafikia waathirika ambao wengi ni wakimbizi wa ndani.Katika ziara hiyo amekutana na wakimbizi wa ndani, viongozi wa kijamii na pia wakuu wa serikali wa eneo hilo.

(SAUTI MAMABOLO)

“UNAMID imekuwa ikifanya jukumu kubwa kusaidia jitihada za serikali katika kutatua migogoro ambayo unakumbana nayo hapa, na kuna haja kubwa ya UNAMID kuendeklea na jukumu hilo kusaidia”