Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yatiwa hofu watoto kufukuzwa shule Burundi

UNICEF yatiwa hofu watoto kufukuzwa shule Burundi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema lina wasiwasi mkubwa juu ya vitendo vya wtoto kukamatwa, kuondolewa shuleni na hata kujeruhiwa huko nchini Burundi. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(Taarifa ya Grace)

Mkurugenzi wa UNICEF, kanda ya kusini na mashariki mwa Afrika, Leila Gharagozloo-Pakkala amesema zaidi ya watoto 300 wamefukuzwa shule na wawili wameripotiwa kujeruhiwa kwa risasi wakati wa maandamano.

Bi. Gharagozloo-Pakkla amesema watoto wote nchini Burundi wana haki ya kupata elimu na kufanya mitihani yao ijayo katika mazingira salama, yaliyolindwa na yasiyoshikiliwa na upande wowote.

UNICEF imetoa wito kwa pande zote kinzani nchini Burundi kuhakikisha zinaheshimu haki ya mtoto kupata elimu na kulindwa dhidi ya ghasia.